walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi

Scan the qr code to link to this page

Hadithi
Ufafanuzi
Kuonyesha Tarjama
Katika Faida za Hadithi
Aina tofauti
Ziada
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.
Ni nzuri - Imepokelewa na Ahmad

Ufafanuzi

Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwenda Aya zingine mpaka wawe wamekwishajifunza elimu liyopo kwenye hizo Aya kumi, na wanazifanyia kazi, hivyo wakajifunza elimu pamoja na kuifanyia kazi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na pupa yao ya kujifunza Qur'ani.
  2. Kujifunza Qur'ani kunakuwa kwa kujifunza na kufanyia kazi yaliyopo ndani yake na kuyafanyia kazi, na siyo kuisoma na kuihifadhi peke yake.
  3. Elimu inakuwa kabla ya maneno na vitendo.

Aina tofauti

Umefanikiwa kutuma