Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}

Scan the qr code to link to this page

Hadithi
Ufafanuzi
Kuonyesha Tarjama
Katika Faida za Hadithi
Aina tofauti
Ziada
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}.
Sahihi - Imepokelewa na Abuu Daud

Ufafanuzi

Anaweka wazi Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Sura za Qur'ani tukufu zilikuwa zikiteremka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haikuwa ikijulikana kitenganishi chake wala mwisho wake mpaka imteremkie: {Bismillahir Rahmanir Rahiim} basi wakati huo ndipo hujua kuwa Sura iliyotangulia imekwisha, na hiyo Bismillahi ni mwanzo wa Sura mpya.

Katika Faida za Hadithi

  1. Bismillah hutumika kuzitenganisha Sura, isipokuwa kati ya Suratul Anfaal na Suratu t-taubah.

Aina tofauti

Umefanikiwa kutuma