Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote

Scan the qr code to link to this page

Hadithi
Ufafanuzi
Kuonyesha Tarjama
Katika Faida za Hadithi
Aina tofauti
Ziada
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy, ameiwekea maelezo kwa njia ya mkato

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na pupa kubwa ya kumtaja Allah Mtukufu, nakuwa yeye alikuwa akimtaja Allah Mtukufu katika nyakati zote mahala popote na katika hali zote.

Katika Faida za Hadithi

  1. Hakuna sharti la twahara ya hadathi ndogo na kubwa kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akidumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Himizo la kukithirisha kumja Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati zote kwa kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, isipokuwa katika hali ambazo zinakatazwa ndani yake kufanya hivyo, kama kukidhi haja.

Aina tofauti

Umefanikiwa kutuma